Kukombolewa kutoka katika upendeleo.

Sawa! Awali Kanisa lilikataa kuwapa daraja la upadre wanawake.
Lakini kwa nini?
Tunapotathmini matukio ya kale ya Kanisa, hatuna budi kuzingatia sababukwa nini vitu vilifamyika jinsi vilivyofanyika. Kwa upande wa wanawake, tuliyoyagundua yanatisha. Wanawake walitengwa kutoka kwenye shughuli za kikuhani bila sababu za halali kabisa.<
The evil of prejudice
Upendeleo wa aina tatu uliwazuia wanawake kutokufanya shughuli za kikuhani.

1. Wanawake walichukuliwa kuwa wa chini katika myanja zote: kimaumbile, kiakili na kihisia.
Kwa kuwa iliaminika kwamba ni mbegu za kiume tu 'zilizokuwa' na mtoto mtarajiwa,wanawake walichukuliwa kama viumbe visivyokamili.
Kwa kifupi wanawake walichukuliw kuwa duni..

2. Kwa kuwa Hawa alisababisha mwanadamu kupoteza neema, kila mwanamke alidhaniwa kuwa amebeba laana ya dhambi yake.
Manawake walichukuliwa kama viumbe wenye dhambi.

3. Watu walidhani kuwa hedhi ya mwanamke humfanya najisi.
Kama viumbe najisi, wanawake walitengwa wasikaribie madhabahu na ibada takatifu./td>

 
Kanisa lahitaji daima kujikomboa lenyewe kutoka kwenye upendeleo wa kijamii na kitamaduni unaodhuru mafundisho na maisha yake.

Hadi mwaka 1854, mapapa walifundisha kwamba Mungu aliruhusu utumwa, jambo ambolo kwa sasa haliruhusiwi kabisa na Kanisa.


Kanisa limefanya makosa mengi ya namna hiyo hiyo wakati wote katika historia yake.

Leo hii wanawake wanahitaji kukombolewa kutoka kwenyeupendeleo wa mafundisho ya kanisa ambao bado yanawazuia kushiriki katika shughuli za kikuhani ambazo ni zao katika mpango wa kweli wa Mungu.


 
  Go to the next step?

1

2

3

4

5

6

7

baptised

empowered

liberated

ordained

affirmed

supported

called